Bembea Ya Maisha Maswali Na Majibu
1. Anwani bembea ya Maisha inaafiki tamthiliya hii. Jadili kwa kutoa hoja ishirini (alama 20)
2. Kwa kurejelea tamthilia hii eleza namna mila na desturi zinavyoweza kuzua migogoro katika jamii. (alama 20)
3. A. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali. "La! Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani akijua itamfaa tena. Kinacholelewa hakina budi kulea."
a) Fafanua muktadha wa mancno haya. (alama 4)
b) Taja mbinu nne zilizotumika hapa. (alama 8)
c) Eleza sifa nne za mnenaji (alama 8)
4. A. Soma dondoo kisha ujibu maswali. "Kumbuka, mrina haogopi nyuki. Marehemu mamangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi mwanadamu wala hazipotei bure — humalizwa tu na mabuu. Mwanangu, usifanye hofu. Nikujuavyo mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. yote yana kikomo ati! Ipo siku haya yote yatapita. Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safl kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka."
a) Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b) Fafanua sifa moja ya mnenaji inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
c) Fafanua mbinu zilizotumika (alama 8).
d) Onyesha kuwa msemewa hakuingia bahari ambayo si yake (alama 6)
5. Soma dondoo kisha ujibu maswali. Eti alama! My foot! Eti ameshuka nafasi darasani lakini akapandisha alama...
a) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
b) Jadili sifa tano za mnenaji. (alama 10)
c) Tathmini umuhimu wa mnenaji katika tamthilia. (alama 8)
6. Soma dondoo kisha ujibu maswali. “Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli,: Hata wahudumu wenyewe hawana mlahaka mwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama UUguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka katika sala”.
a) Changanua mtindo wa dondoo kwa kurejelea hoja tano. (alama 10)
b) Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. (alama 10)
7. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali. ‘...wanajikuta katika vuta n'kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani, ushirikiano, upendo, kutanabahi, na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara.. ."
a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)
b) Hakiki mtindo wa dondoo hili. (alama 2)
c) Fafanua mitikiso saba inayotishia mahusiano ya kijamii ya tamthilia hii. (alama 14)