BUY NOW
KSh.190
Mapambazuko Ya Machweo Maswali na Majibu

Mapambazuko Ya Machweo Maswali na Majibu

KCSE Setbooks Notes
37872 viewers
Reading Time:

 1. Fafanua changamato wanazokumbana nazo waajiriwa katika hadithi Harubu ya   Maisha (alama 20) 

 

2. Jadili matumizi ya pombe haramu na athari zake katika hadithi kila mchezea wembe (alama 20) 

 

3. Fafanua wa ufaafu wa anwani Fadhila za Punda (alama 20) 

 

4. Fafanua dhiki zinazowakumba raia katika hadithi ya Msiba za Kujitakia (alama 20) 

 

5. Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Machweo (alama 20) 

 

6. Urumo umekita mzizi katika jumuiya ya Mapambazuko ya Machweo. Jadili ( alama 20 )

 

7. Miti katika misitu ilizidi kuangamizwa kwa makali ya shoka lakini miti ilizidi kulifurahia shoka...miti ikafikiri shoka ni mmoja wao!"   

 

a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)   

b) Bainisha mbinu zozote mbili katika mkutadha huu. (alama 4)   

c) Eleza sifa mbili za shoka. (alama 2) 

d) Kwa kurejelea hadithi ya msiba wa kujitakia, jadili mbinu zinazotumiwa na   viongozi kuingia mamlakani. (alama 10)

 

8. "tafadhali nisamehe...ni barua ilinikawiza..."   

 

a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)   

b) Tambua kipengele kimoja cha kifani kilichotumiwa katika dondoo hili.  (alama 2)   

c) Eleza barua hii na matokeo yake. Alama 6)   

d) Jadili dhima ya msemaji katika kuendeleza maudhui ya hadithi. (alama 4)   

e) Fafanua namna wahusika wote wawili walivyochangia kumwauni   msemaji. (alama 2) 

 

9. a) Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, jadili changamoto zinazokumba   asasi ya ndoa. (alama 5)   

 

b) Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, fafanua matatizo   yanayowakumba wafanyikazi. (alama 10)   

 

c) Jadili dhana ya utatu inavyojitokeza katika diwani ya mapambazuko ya   machweo na hadithi nyingine. (alama 5)   

 

10...iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa   penzi langu kama jongoo na mti wake..." 

 

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b) Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (alama 4)   

c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)   

d) Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alama 6) 

 

11. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii. (alama 20)   

i. Toba ya kalia   

ii. Ahadi ni deni   

iii. Nilitamani   

iv. Pupa 

 

12.Wanaume katika mataifa mengi barani afrika wametawaliwa na ubabedume.   Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya "Fadhila za Punda" (al.20)

 

13.Huku ukitolea mifano mwafaka ,eleza jinsi ambavyo haki za watoto/vijana   zimekiukwa katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo 

 

14.Mwandishi katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia alifaulu kutumia mbinu ya uwili. Thibitisha. (al. 20)

 

15.Mwandishi wa hadithi ya "mapambazuko ya machweo" uwajibikaji kwa kiasi   kikubwa mno. Illihirisha ukweli na kauli hii (al.20)

 

16.Wafanyikazi katika nchi nyingi zinazoendelea wanakumbwa na changamoto nyingi sana. Thibitisha hali hii kwa kurejelea hadithi ya " harubu ya 20) 

 

17.Ukombozi wa wanawake unakumbwa na vizingiti vingi sana. Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya sabina. (al. 20) 

 

18.Fafanua dhana ya ajira katika hadithi Mapambazuko ya Machweo (alama 20) 

 

19. “mwanangu, nizike duniani unifunike…”   

 

a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (al.4)   

b) Taja na utolee mfano mbinu moja ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili (al.2) 

c) Ukirejelea hadithi ya" Mzimu wa Kipwerere," fafanua jinsi imani katika  mambo ya kichawi yamejikita katika jamii. (al. 14) 

 

20.Fafanua jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika hadithi ya Nipe Nafasi (alama 20) 

 

21. "thank you. U mteja wa pekee, unajua kuthamini huduma nzuri unapopewa."   

 

a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al.4)   

b) Taja na ueleze mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili. (al.4)   

c) Kwa kurejelea hadithi ya "kila mchezea wembe," fafanua changamoto   zinazowakumba watumiaji wa vileo kupita kiasi. (al. 12)

 

22. "...iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa   penzi langu kama ongoo na mti wake...   

 

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)   

b) Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (alama 4)   

c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)   

d) Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (alam 6) 

 

23.Kwa kurejelea hadithi ya Ahadi ni Deni, fafanua namna uwajibikaji umejitokeza. (alama 20) 

 

24."kwa kweli, nimeungulika sana miaka yote hii kwa unyama tuliomtendea Jack.. ."   

 

a) eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)   

b) jadili umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. (alama 6)   

c) jadili ukatili aliokuwa ametendewa mhusika jack kulingana na dondoo hili.   (alama 5)   

d) kwa kurejelea mhusika jack, jadili maudhui ya nafasi ya vijana. (alama 5) 

 

25.Onyesha namna mwandishi wa hadithi ya nipe nafasi alivyodokeza maudhui ya   taasubi ya kiume. (alama 20) 

 

26.Ndoa ni taasisi iliyokuzwa katika hadithi fadhila za punda. Fafanua (alama 20) 

 

27....wajua siku hizi huwezi kuamini yeyote apitaye na hasa akiomba msaada au   umekula kututapeli?"   

 

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)   

b) Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya katika kujenga maudhui   kwenye hadithi hii. (alama 10)   

c) Eleza sifa za msemaji wa maneneo haya. (alama 5) 

 

28.Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii.   (alama 20)   

 

a) Toba ya kalia   

b) Ahadi ni deni   

c) Nilitamani   

d) Pupa   

 

29.Rachel wangari katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo ametumia mbinu   ya jazanda kwa upana. Jadili (alama 20) 

 

30.Swala la elimu limepewa kipaumbele katika hadithi ya Sabina. Jadili (alama 20) 

 

31.Fafanua jinsi yusuf shoka hamad katika hadithi mzimu wa   kipwerereameshughulikia swala la ushirikina na unafiki (alama 20)

 

32.Umaskini ni donda sugu katika hadithi kifo cha suluhu, huku ukitoa hoja ishirini jadili (alama 20) 

 

33.Eleza jinsi ubabedume umejitokeza katika hadithi ya Nipe Nafasi (alama 20)

 

Mathematics Form 2 Notes
MORE RELATED MATERIALS View All
Fathers Of Nations Questions & Answers 1) Discuss the relevance of the Title ‘Fathers of Nations ‘by Paul B.Vitta (20 marks) 2) Effective leadership guarantees its people security and equitable distribution of resources and opportunities, discuss the irony of this statement basing your arguments on the novel fathers of nation by Paul B, Vitta (20 marks)
Published on:31/05/2023
Maswali ya Marudio 1. "Aah, si mnajua wale watu ni hatari. Lakini hawatakuwa na nguvu tena. Njia zao zote nitazifunga..." a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) b. Jadili hatari zilizosababishwa na watu wanaorejelewa na msemaji. (alama 10) c. Msemaji ananuia kuzifunga njia za warejelewa vipi? (agama 6).
Published on:30/05/2023
1. Anwani bembea ya Maisha inaafiki tamthiliya hii. Jadili kwa kutoa hoja ishirini (alama 20) 2. Kwa kurejelea tamthilia hii eleza namna mila na desturi zinavyoweza kuzua migogoro katika jamii. (alama 20)
Published on:30/05/2023