BUY NOW
KSh.200
Nguu Za Jadi Maswali Na Majibu

Nguu Za Jadi Maswali Na Majibu

KCSE Setbooks Notes
56082 viewers
Reading Time:

Maswali ya Marudio

 

1. "Aah, si mnajua wale watu ni hatari. Lakini hawatakuwa na nguvu 

tena. Njia zao zote nitazifunga..." 

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Jadili hatari zilizosababishwa na watu wanaorejelewa na msemaji. (alama 10)

c. Msemaji ananuia kuzifunga njia za warejelewa vipi? (agama 6). 

 

2. "Hakika kila mtu ni mhusika mkuu katika kisa cha maisha yake mwenyewe. Hivyo, ni furaha kubwa kwa mhusika huyo kuipa hadhira yake kitu cha kuwatia moyo maishani..." 

a. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Mhusika katika dondoo hili ameipa hadhira yake kitu gani cha kuwatia moyo? (alama 16)  3. "Mwanao? Mimi mwanao mimi? Tangu siku ile uliyonila kivuli, mimi si mwanao tena..."  a. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)

b. Tambua na ueleze tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4) 

c. Eleza namna wahusika katika dondoo hili wanavyoendeleza maudhui ya ukengeushi.  (alama 12) 

 

4. "Alifunzwa kutotumia sifa zake za kike alizokirimiwa na Muumba kustarehesha wanaume ili kujinufaisha kimaisha..." 

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Kwa kurejelea riwaya nzima, onyesha jinsi anayerejelewa katika dondoo hili alivyojikomboa kimawazo. (alama 8) 

c. Kwa kutoa mifano, onyesha jinsi baadhi ya wahusika wa kike wanavyotumia sifa za kike kujinufaisha kutokana na wanaume. (alama 8) 

5. "Yapimeni maneno ya Mbungulu. Hata kama tuna ushahidi huu, tangu lini panya akashinda kesi mbele ya baraza la paka?" 

a. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Je, panya na paka wanaorejelewa ni akina nani, na pana kesi gani? (alama 6) 

c. Onyesha jinsi akina 'panya' walivyonyimwa haki na akina 'paka' katika riwaya hii. (alama 10) 

 

6. "Mrima, dunia yote inajua aliyemsaliti Yesu Kristo. Unajua mtu huyo aliishia wapi?"  a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Tambua na ufafanue umuhimu wa mbinu ya uandishi inayojitokeza katika dondoo. (alama 2) 

c. Kwa kurejelea riwaya nzima, onyesha jinsi ambavyo mwandishi anashughulikia maudhui ya usaliti. (alama 14) 

 

7. "Lazima sasa atimize alilonuia. Hilo lilibeba hatima ya kila mtu Matango..."  a. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Anayerejelewa katika dondoo hili ananuia kutimiza kitu gani? (alama 4)  c. Kwa nini hatima ya kila mtu inategemea lile alilonuia kufanya mrejelewa? (alama 12) 

 

8. "Mangwasha, siku zote hizi ulikuwa unachezeshwa kayamba tu..." 

a. Andika muktadha wa maneno haya. (alama 4) 

b. Nani anamchezesha kayamba na kwa nini? (alama 8) 

c. Eleza shida anazopitia msemaji wa maneno haya. (alama 8) 

 

9. "Tafadhali usiende huko...sasa unanifananisha mimi na..." 

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Eleza sababu zinazomfanya msemaji kutamka maneno hayo. (alama 6)  c. Jadili umuhimu wa msemaji katika riwaya hii. (alama 10) 

10. "Hakuna heshima wala utu. Yaani kwa ufupi, tumevaa silika za wanyama.,."  a. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Thibitisha kuwa wahusika wengi katika riwaya hii wamevaa silika za wanyama. (alama 16) 

 

11. "Ama kweli, wavuvi wa juya huiendea bahari ya hadhi Yao..." 

a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

 

b. Tambua na ufafanue sitiari iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)  c. Wavuvi wanaorejelewa wamesababisha maafa gani katika jamii? (alama 12) 

 

12. Eleza namna maudhui ya tamaa na ubinafsi yalivyoshughulikiwa katika riwaya hii.  (alama 20) 

 

13. Eleza jinsi mhusika Sagilu anavyosawiriwa katika riwaya hii. (alama 20)  14. Fafanua jinsi utabaka unavyojitokeza katika riwaya hii. (alama 20) 

 

15. Jadili jinsi mabadiliko yanavyojitokeza katika maisha ya wahusika Mashauri na Ngoswe.  (alama 20) 

 

16. Onyesha namna Lonare anavyoendeleza maudhui ya uvumilivu. (alama 20) 

 

17. Fafanua jinsi mwandishi anavyotumia mbinu ya kisengerenyuma katika riwaya hii.(alama 20) 

 

18. Jadili matumizi ya taharuki kama yanavyojitokeza katika riwaya hii. (alama 20)  19. Fafanua sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao. (alama 20) 

a. Sihaba 

b. Mwamba 

c. Mrima 

d. Chifu Mshabaha 

 

20. Mtemi Lesulia ni adui wa maendeleo ya Matuo. Fafanua ukweli wa kauli hii. (alama 20)

 

21. 'Ibilisi wa mtu ni mtu.' Jadili ukweli wa usemi huu kwa kurejelea wahusika wanne katika riwaya hii. (alama 20) 

 

22. Cheiya ni mfano wa kuku ambaye anakimbilia punje za mpunga. Fafanua ukweli wa kauli hii. (alama 20) 

 

23. Taja nguu ambazo zinatokana na jadi na ueleze jinsi zinavyovunjwa katika riwaya hii.  (alama 20) 

 

24. Huku ukitoa mifano, onyesha jinsi mwanamke anavyodunishwa katika riwaya hii. (alama 20) 

 

25. Mrima ni kielelezo cha matatizo yanayoikumba ndoa ya kisasa. Jadili. (alama 20)  

 

26. Eleza umuhimu wa mhusika Mangwasha katika riwaya hii. (alama 20)  

 

27. Mwandishi amefaulu kutumia kinaya kufanikisha dhamira yake. Jadili. (alama 20) 

 

28. Jadili mchango wa utamaduni katika ama kuiendeleza jamii au kudumaza maendeleo.  (alama 20) 

 

29. "Laiti wangalivuta fikira zaidi, wangalijua chanzo cha mateso Yao..."  a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b. Eleza umuhimu wa mzungumzaji wa kauli hii katika kuijenga riwaya hii. (alama 16)  30. Jadili namna masuala yafuatayo yanavyoshughulikiwa katika riwaya.  a. Utabaka (alama 5) 

b. Ufisadi (alama 5) 

c. Ukombozi (alama 5) 

d. Afya ya kiakili (alama 5) 

 

Mathematics Form 2 Notes
MORE RELATED MATERIALS View All
Fathers Of Nations Questions & Answers 1) Discuss the relevance of the Title ‘Fathers of Nations ‘by Paul B.Vitta (20 marks) 2) Effective leadership guarantees its people security and equitable distribution of resources and opportunities, discuss the irony of this statement basing your arguments on the novel fathers of nation by Paul B, Vitta (20 marks)
Published on:31/05/2023
1. Anwani bembea ya Maisha inaafiki tamthiliya hii. Jadili kwa kutoa hoja ishirini (alama 20) 2. Kwa kurejelea tamthilia hii eleza namna mila na desturi zinavyoweza kuzua migogoro katika jamii. (alama 20)
Published on:30/05/2023
1. Fafanua changamato wanazokumbana nazo waajiriwa katika hadithi Harubu ya Maisha (alama 20) 2. Jadili matumizi ya pombe haramu na athari zake katika hadithi kila mchezea wembe (alama 20) 3. Fafanua wa ufaafu wa anwani Fadhila za Punda (alama 20) 4. Fafanua dhiki zinazowakumba raia katika hadithi ya Msiba za Kujitakia (alama 20) 5. Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Machweo (alama 20)
Published on:31/05/2023